PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 18, 2015

YOUNG AFRICANS HISTORY IN KAGAME CUP || OPENING MATCH SINCE 1993


Ndugu wananchi, ni wazi na ukweli usiofichika kwamba hakuna mashabiki wanaofurahi timu yao kufungwa. Lakini kufungwa mechi ya kwanza ni NEEMA kuliko kufungwa mechi ya mwisho. Historia inainesha hivyo. Mechi za awali zinatuamsha usingizini kisha tunaanza kwenda kwa kasi kama treni inavyoshuka kutoka mlimani ikiwa imekatika breki.
- Nani kasahau kwamba msimu ulioisha tuliobeba Ubingwa tulianza kwa sare kisha tukacharazwa 3-0 na Mtibwa Sugar.
- Nani kasahau kwamba hata msimu kabla ya Azam FC kubeba ubingwa tulianza hivi hivi kwa kucharazwa na hao hao Wana-Manungu?

SASA TUANGALIE HISTORIA YETU YA KAGAME CUP
Mwaka 1993: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni Uganda, mechi ya kwanza tulifungwa 3-1 na wenyeji SC Villa tukakutana nao fainali tukawapiga 2 - 1, ndoo ikatua Jangwani.
Mwaka 1999: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni wale wale Uganda, mechi ya kwanza tulifungwa na Rayon Sports ya Rwanda mabao 3 - 0, tukaingia fainali na SC Villa tukashinda kwa penalties na shujaa akiwa ni Peter Manyika Sr. (Baba ake huyu kipa wa Mkia)
Mwaka 2011: Tanzania tukiwa wenyeji wa Kagame Cup, mechi ya kwanza tukatoa 2 - 2 na vigogo El Merreikh ya Sudan, tena magoli manne walifunga wachezaji wa El Merreikh. Fainali tukaingia na Wazee wa Mikataba Feki, tukawabanika 1 - 0, bao la Asamoah kufuatia krosi ya Kigi Makassy.
Mwaka 2012: Tanzania wakiwa wenyeji kwa mwaka wa pili mfululizo, mechi ya kwanza tukapigwa 2 - 0 na Atletico ya Burundi, Kavumbagu akiwa na timu hiyo akitupia na kutuadhibu. Fainali tukaingia Koni Chapati aka Azam FC tukawakalisha bao 2 - 0. Magoli ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi
Mwaka huu 2015: Tanzania wenyeji tena, mechi ya kwanza leo tumefungwa 2 - 1 na Gor Mahia ya Kenya.
WALE WANANCHI WOTE AMBAO BADO WANA IMANI NA TIMU YETU KAMA MIMI ADMIN WENU TUGONGE LIKE. WALE WASIO NA IMANI KAENI KIMYA TU.

VIMECHI VIWILI TU NO COMPLICATION


TUJARIBU KUANGALIA MIKEKA YA MISIMU ILIYO PITA


nini hatima ya Arda Turan baada ya barcelona kulamba rungu la fifa?

Inasemekana mchezaji Arda Turan aliyesajiliwa na Barcelona msimu huu wa usajili akitokea Athletico Madrid anaweza patikana kwa mkopo wa miezi sita kwa timu itakayo hitaji huduma yake.
Liverpool pia ambao wamekuwa wakimuwinda mchezaji huyo wanaweza mpata Arda Turan kwa mkopo wa miezi sita kwa kuwa hatoweza chezea Barcelona mpaka ipite miezi sita hii inatokana na adhabu waliyopewa na fifa.
Adhabu hiyo inaisha 2016 hivyo itamfanya mchezaji huyo aanze kuitumikia timu hiyo.
Kwa kuwa ni ngumu kwa mchezaji kariba ya turan kukaa nje ya timu kwa miezi sita bila kucheza watafiti wa mambo wanasema anaweza tafuta timu akacheza kwa mkopo wa miezi sita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema ni vigumu yeye kukaa nje miezi sita hivyo hivi sasa anakabiriwa na maamuzi magumu aidha kubaki camp nou na kufanya mazoezi au kwenda timu nyingine kwa mkopo kwani anachokihitaji ni kuuzoea mfumo wa barca na mazingira yake.
Arda Turan inasemekana amenunuliwa kuchukua nafasi ya xavi ingawa ni wachezaji wawili tofauti ambao wanatofautiana kiuchezaji na sasa Enrique Luis ana kazi ya kumfanya mchezaji huyo aendane na mastaa wa timu hiyo.
Ngoja tuone atachagua nini kijana huyu wa kituruki,atakua wapi ndani ya miezi sita ni jambo la kusubiri.

Jul 17, 2015

Ipi ni njia nzuri ya kubeti(betting)?


Watu wengi wakisikia neno bet, moja kwa moja wanahuisha na mpira wa miguu, ni kweli wapo sawa ila betting siyo kwenye mpira wa miguu tu hata kwenye michezo kama cricket, basketball, ngumi na michezo mingine. Embu tungalie kwa upande wa mpira wa miguu ambo unaongoza kwakua na mashibiki wengi duniani. Kwa hapa Tanzania kuna makampuni mengi yanayo jihusisha na mechezo ya kubahatisha/bahati nasibuu mfano wa makampuni hayo ni m-bet a meridian ambayo yanaongoza kuwa na wateja wengi.
Tuangangalie kwa uande wa m-bet. Ukifuata hatua hizi utaweza kuwa unashinda katika ubashiri utakaofanya :-
1. usiweke mechi nyingi kwa mkeka mmoja/ticket. Hii ni kwasababu unapoweka mechi nyingi katika mkeka mmoja unapunguza uwezekano wa wewe kushinda. Japo kuwa wengi wanawaza kupata hela nyingi lakini wanasahau kuangalia uwezekano wa kushinda. Ni kweli kwamba ukiweka mechi nyingi ndio hela inaongezeka ila uwezekano wakushinda unapungua, ndiyo maana wenye makampuni hawaruhusu kubeti/kutandika mkeka wa mechi moja .angallia mfano hapo chini

2. Zijue timu unazozibetia/ ambazo unazitabiria : kujua timu kabla ya kubeti ni jambo muhimu sana kwa sababu kunatimu ni mahasimu sana katika ligi fulani. Kwa mfano ligi kuu vodacom wakicheza simba na yanga, hata kama simba akiwa anashika nafasi za mwishoni katika ligi hatakubali kufungwa kirahisi na yanga kwa hiyo mechi itakua naupinzani mkali. Mara nyingi zikikutana timu kama hizi matokeo huishia kuwa droo/draw au utofauti mdogo wa magoli kwa mfano mechi inaweza kuisha 0-0, 1-1, 2-2, na sare nyinine au 1-0, 0-1, 2-1, 3-2. kwahiyo kwa timu kama hizi usibeti kwamba timu fulani itashinda kwa tofauti ya magoli mawili au zaidi. Pia kingine atika kuzijua timu jaribu kuangalia kama kuna timu ni kibonde wa mwingine. Kwa mfano asernal ni mteja wa man united mara kwa mara, kwahiyo jaribu kuangalia nani anamfunga mwenzake mara kwa mara kisha mpe.


3.usibetie timu kwa sababu ya ushabiki: hiki ni kitu cha kuzingatia kwani wengi wwamekua wakibet kwa sababu tu ya mapenzi ya katika timu fulani. Ushauri ni bora usibetie timu unayoipenda kama uwezi kazuia hisia zako, kwani hisia zinamzuia mtu kuichambua timu anoyo ishabikia

4.Angalia goal differences/ tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa: ni vizuri kuangalia tofauti ya magoli kwa zile timu ambazo unataka kuzibetia na hii ni nzuri hususani kwa wale ambao watakua wanabeti kama timu zote zitafunga. Kwa mfano kama timu inamagoli mengi ya kufunga kuliko ya kufungwa ni wazi kwamba timu hii haifungwi mara kwa mara kwa hiyo ikikikutana/kucheza na timu ambayo ina magoli mengi sana ya kufugwa kuliko ya kufunga, hii inaonyesha kuwa hii timu itafungwa bila yenyewe kufunga kwahiyo kama uliweka both team will score “yes” huo mkeka utakua umechanika.
NB: hii haimanishi kwamba itakua hivyo kwa mechi zote ila ni kwamba uwezekano mkubwa/ possibility ipo hivyo 

5. Cheza kwa kiasi mchezo huu. Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, hutaumia. Jaribu kuweka mikakati na mipangilio juu ya uchezaji wako, hakika hutajuta. Cheza mechi chache kwa siku unazoamini zinaweza kukupatia ushindi sio lazima ubashiri mechi nyingi kwa mkupuo. Hii itakusaidia wewe kukupa ushindi mara nyingi

6. Usibashiri kwa mapenzi ama ushabiki, eti kwa kuwa mimi ni mshabiki wa liverpool Fc basi ndo nakuwa naitabiria ushindi kila mara, angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri