PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 18, 2015

nini hatima ya Arda Turan baada ya barcelona kulamba rungu la fifa?

Inasemekana mchezaji Arda Turan aliyesajiliwa na Barcelona msimu huu wa usajili akitokea Athletico Madrid anaweza patikana kwa mkopo wa miezi sita kwa timu itakayo hitaji huduma yake.
Liverpool pia ambao wamekuwa wakimuwinda mchezaji huyo wanaweza mpata Arda Turan kwa mkopo wa miezi sita kwa kuwa hatoweza chezea Barcelona mpaka ipite miezi sita hii inatokana na adhabu waliyopewa na fifa.
Adhabu hiyo inaisha 2016 hivyo itamfanya mchezaji huyo aanze kuitumikia timu hiyo.
Kwa kuwa ni ngumu kwa mchezaji kariba ya turan kukaa nje ya timu kwa miezi sita bila kucheza watafiti wa mambo wanasema anaweza tafuta timu akacheza kwa mkopo wa miezi sita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema ni vigumu yeye kukaa nje miezi sita hivyo hivi sasa anakabiriwa na maamuzi magumu aidha kubaki camp nou na kufanya mazoezi au kwenda timu nyingine kwa mkopo kwani anachokihitaji ni kuuzoea mfumo wa barca na mazingira yake.
Arda Turan inasemekana amenunuliwa kuchukua nafasi ya xavi ingawa ni wachezaji wawili tofauti ambao wanatofautiana kiuchezaji na sasa Enrique Luis ana kazi ya kumfanya mchezaji huyo aendane na mastaa wa timu hiyo.
Ngoja tuone atachagua nini kijana huyu wa kituruki,atakua wapi ndani ya miezi sita ni jambo la kusubiri.

No comments:

Post a Comment