PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 19, 2015

NGOMA HAJAFANYA KOSA KUBWA

Soka ni mchezo wenye mengi sana uwanjani, baadhi ya wachezaji huitafutia ushindi timu yao kwa namna yoyote ile iwe nzuri ama mbaya!baadhi hujiangusha maksudi kumdanganya refa atoe penati wengine hufunga hata magoli ya mkono yote ni kuhakikisha timu yake itoke na ushindi tu . . Wengine hutumia njia za kuwarubuni wenzao kuwakasirisha ndipo refa atoe adhabu!
Tulishuhudia katika fainali ya kombe la dunia 2006(10 june),Zidane akimpiga kichwa Marco Matterazi ikisemekana kuna maneno aliambiwa , juzi tu hapa katika COPA-America Edson Cavan alilimwa kadi nyekundu kwa kumzaba kibao Gonzalo Jara wengi walimlaumu lakini baada ya marudio ikaonekana Jara akimtia kidole Cavan kama ilivyo kwa tukio la Maguli na Juma Nyoso.
Baada ya kuisumbua vilivyo safu ya ulinzi ya Gor Mahia,ndipo Haroun Shakava akaamua kucheza na hisia za Donald Dombo Ngoma.Beki huyo alimparamia maksudi Donald Ngoma nje ya uwanja ambaye alishindwa kudhibiti hasira zake na kumsukuma kwa jazba Shakava,refa akamuonesha kadi nyekundu Ngoma ikawa heri kwa Shakava pamoja na timu nzima ya Gor Mahia.
Donald Ngoma alitoka akiwa analia,anajutia kwa kushindwa kudhibiti hasira zake mbaya zaidi ni mchezo wake wa kwanza kimashindano kuichezea Yanga,alilia akijua wazi jinsi gani alivyoigharimu timu yake ikiwa dakika ya 24 tu kipindi cha kwanza.
Tunapata nafasi muhimu ya kusawazisha lakini Nadir Haroub Captain anapiga penati ya madoido 'panenka" inagoma,ndio penati ile ile aliyopiga dhidi ya Al - Ahly tuliyomsifia na kuchekelea kuwa anajua lakini jana ikawa tofauti!
Baada ya mchezo kocha wetu Hans Van Pluijm alisema kuna mambo benchi lake la ufundi na wachezaji wamejifunza katika mchezo huo,nnachokiona kwa haraka Donald Ngoma amepata funzo hata Cannavaro kuna kitu kajifunza!Mashabiki wenzangu tujifunze kuwapenda wachezaji wetu katika hali zote na kwa usawa,nawaza tu angekuwa Simon Msuva aliyepewa kadi nyekundu au kukosa penati sijui ingekuaje hapo jana?
Tuonane Jumatano Uwanja wa Taifa saa 10 jioni dhidi ya Telecom ha Djibout.

No comments:

Post a Comment