PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 13, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 13.07.2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 13.07.2015
Juhudi za Manchester City kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba zimekwama kutokana na mkataba wa hakimiliki wa picha za mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Pogba pia ataomba kuondoka ili kukamilisha uhamisho huo (Daily Star), Meneja wa Chelsea Jose Murinho anataka kumsajili Pedro, 27 kutoka Barcelona (Sport), Paris Saint-Germain wanataka kumsajili Angel Di Maria kutoka Manchester United, lakini meneja Laurent Blanc anasema itakuwa vigumu kwa sababu timu nyingi zinamtaka (L'Equipe), Manchester United wapo tayari kuzuia uhamisho wa David De Gea kwenda Real Madrid, vinginevyo mkataba ufikiwe kabla Man United hawajakwenda Marekani (Sun), Southampton wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Uholanzi Jordy Claise, 24, kuziba pengo la Morgan Schneiderlin anayeelekea Manchester United (Sun), Newcastle wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo kutoka Uholanzi Georginio Wijnaldum, 24 kutoka PSV Eindhoven (Guardian), meneja wa Aston Villa, Tim Sherwood amempongeza nahodha Fabian Delph kwa kuamua kusalia Villa badala ya kwenda Manchester City (Birmingham Mail), wakala wa Victor Valdes anasema kipa huyo anataka kusalia Manchester United, licha ya kuhusishwa na kuhamia Antalyaspor ya Uturuki (AS), rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesema atamuuza mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain ambaye pia amehusishwa na kuhamia Arsenal, iwapo kitita cha pauni milioni 64.7 kitatolewa (Daily Express), QPR watapata pauni milioni 9 kama mgao kwa mauzo ya Raheem Sterling kutoka Liverpool kwenda Manchester City. Winga huyo, 20, alisajiliwa na Liverpool kwa pauni laki tano mwaka 2010 (Daily Mail), Liverpool wanazungumza na Fiorentina kutaka kumchukua Mario Gomez, na wapo tayari kumtoa Mario Balotelli- wote kwa mkopo (Sport Mediaset), Jose Mourinho amezuia uhamisho wa John Obi Mikel kwenda Al-Ain na Al-Wahda za Falme za Kiarabu (BBC), Atletico Madrid wamekataa dau la Manchester United la kumsajili kipa Jan Oblak (AS)
Image result for paul pogba
Image result for valdes









Image result for angel di maria

No comments:

Post a Comment