PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 13, 2015

LIVERPOOL WAPATA FAIDA KUBWA KWA UHAMISHO WA Rahim Sterling

Hapa Liverpool wamepata faida wao ukilinganisha na bei waliyomnunua kutoka timu uliyomlea QPR na ambao watapata mgao wa 10% kama sijakosea mtanirekebisha hapa lakini yote kwa yote Liverpool wamefanya biashara nzuri.
Achilia mbali mchezaji huyo atapaform vipi kwenye timu yake hiyo mpya sababu usajili ni kama pata potea haswa kwa wachezaji wenye umri mdogo kama yeye.
Sterling kama ilivyo kwa wachezaji wote duniani wanahitaji mafanikio na mafanikio ya mchezaji ni kutwaa vikombe na tunzo mbali mbali hivyo basi labda ameona man city ni mahala sahihi kwake kuliko Liverpool ingawa wengi kama ilivyo mimi tunaona amefanya haraka sana kuondoka Liverpool.
Wengi tunakubali uwezo wake na kapaji chake ni miongoni mwa wachezaji wanao jituma sana uwanjani achilia mbali makosa madogo madogo ya kiuchezaji aliyonayo.
Tabia yake na muenendo wake ulibadirika ghafla na kuwakera mashabiki wa Liverpool karibu duniani kote pamoja na management nzima ulisababisha yeye kuuzwa.
Liverpool wamefanya la maana kumuachia mchezaji huyo kwani tayari alishaonyesha hana hamu tena ya kubaki hapo hivyo isengekuwa vema kuendelea nae.
Kwa fedha zilizopatikana inaweza ikanunua mbadala wake ingawa hatofanana na Sterling lakini ataweza ziba pengo hilo au nafasi yake inaweza zibwa vizuri tu na chipukizi anayekuja kwa kasi sana JORDAN IBE endapo hatopelekwa kwa mkopo tena kupata uzoefu zaidi hapa BRENDAN RODGERS atakua na mtihani mwingine ingawa wapo pia kina lazar markovic,adam lalana nao wanaweza ziba hiyo nafasi pia.
Ngoja tuone anaweza fanikiwa na akatimiza malengo yake au asifanikiwe kama alivyodhani wakati mwingine mpira unakua na mambo ya ajabu na kumfanya mtu kuikimbia bahati ndio maisha ya mpira yalivyo.
Yote kwa yote binafsi namtakia mafanikio mema huko aendapo Rahim Sterling na nashukuru kwa mchango wake pia na nasema
 Image result for Raheem Sterling

No comments:

Post a Comment