Watu
wengi wakisikia neno bet, moja kwa moja wanahuisha na mpira wa miguu,
ni kweli wapo sawa ila betting siyo kwenye mpira wa miguu tu hata
kwenye michezo kama cricket, basketball, ngumi na michezo mingine.
Embu tungalie kwa upande wa mpira wa miguu ambo unaongoza kwakua na
mashibiki wengi duniani. Kwa hapa Tanzania kuna makampuni mengi
yanayo jihusisha na mechezo ya kubahatisha/bahati nasibuu mfano wa
makampuni hayo ni m-bet a meridian ambayo yanaongoza kuwa na wateja
wengi.
Tuangangalie kwa uande wa m-bet. Ukifuata hatua hizi utaweza kuwa
unashinda katika ubashiri utakaofanya :-
1.
usiweke mechi nyingi
kwa mkeka mmoja/ticket.
Hii ni kwasababu unapoweka mechi nyingi katika mkeka mmoja unapunguza
uwezekano wa wewe kushinda. Japo kuwa wengi wanawaza kupata hela
nyingi lakini wanasahau kuangalia uwezekano wa kushinda. Ni kweli
kwamba ukiweka mechi nyingi ndio hela inaongezeka ila uwezekano
wakushinda unapungua, ndiyo maana wenye makampuni hawaruhusu
kubeti/kutandika mkeka wa mechi moja .angallia
mfano hapo chini
2.
Zijue timu
unazozibetia/ ambazo unazitabiria
: kujua timu kabla ya kubeti ni jambo muhimu sana kwa sababu kunatimu
ni mahasimu sana katika ligi fulani. Kwa mfano ligi kuu vodacom
wakicheza simba na yanga, hata kama simba akiwa anashika nafasi za
mwishoni katika ligi hatakubali kufungwa kirahisi na yanga kwa hiyo
mechi itakua naupinzani mkali. Mara nyingi zikikutana timu kama hizi
matokeo huishia kuwa droo/draw au utofauti mdogo wa magoli kwa mfano
mechi inaweza kuisha 0-0, 1-1, 2-2, na sare nyinine au 1-0, 0-1, 2-1,
3-2. kwahiyo kwa timu kama hizi usibeti kwamba timu fulani itashinda
kwa tofauti ya magoli mawili au zaidi. Pia kingine atika kuzijua
timu jaribu kuangalia kama kuna timu ni kibonde wa mwingine. Kwa
mfano asernal ni mteja wa man united mara kwa mara, kwahiyo jaribu
kuangalia nani anamfunga mwenzake mara kwa mara kisha mpe.
3.usibetie
timu kwa sababu ya ushabiki:
hiki
ni kitu cha kuzingatia kwani wengi wwamekua wakibet kwa sababu tu ya
mapenzi ya katika timu fulani. Ushauri ni bora usibetie timu
unayoipenda kama uwezi kazuia hisia zako, kwani hisia zinamzuia
mtu kuichambua timu anoyo
ishabikia
4.Angalia
goal differences/ tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa:
ni vizuri kuangalia tofauti ya magoli kwa zile timu ambazo unataka
kuzibetia na hii ni nzuri hususani kwa wale ambao watakua wanabeti
kama timu zote zitafunga. Kwa mfano kama timu inamagoli mengi ya
kufunga kuliko ya kufungwa ni wazi kwamba timu hii haifungwi mara kwa
mara kwa hiyo ikikikutana/kucheza na timu ambayo ina magoli mengi
sana ya kufugwa kuliko ya kufunga, hii inaonyesha kuwa hii timu
itafungwa bila yenyewe kufunga kwahiyo kama uliweka both team will
score “yes” huo
mkeka utakua umechanika.
NB:
hii haimanishi kwamba itakua hivyo kwa mechi zote ila ni kwamba
uwezekano mkubwa/ possibility ipo hivyo
5. Cheza
kwa kiasi mchezo huu. Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi
kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, hutaumia. Jaribu
kuweka mikakati na mipangilio juu ya uchezaji wako, hakika hutajuta.
Cheza mechi chache kwa siku unazoamini zinaweza kukupatia ushindi sio
lazima ubashiri mechi nyingi kwa mkupuo. Hii itakusaidia wewe kukupa
ushindi mara nyingi
6. Usibashiri kwa mapenzi
ama ushabiki, eti kwa kuwa mimi ni mshabiki wa liverpool Fc basi ndo nakuwa
naitabiria ushindi kila mara, angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu
pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa
mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri