Donald Dombo Ngoma mshambuliaji aliyefunga katika kila mchezo toka atue Yanga, atatumikia adhabu ya kadi kwa kukosa mchezo mmoja wa siku ya jumatano dhidi ya Telecom-Djibouti,hata hivyo nafasi yake itazibwa na mchezaji aliye katika kiwango cha juu kwa sasa yaani Kpah Sean Sherman au Malimi Busungu ambao wote ni moto wa kuotea mbali na shughuli zao ni nzito.
Hapo jana kocha wa Kampala City Council Authority (KCCA) alishindwa
kujizuia baada ya mtanange kumalizika alimfuata Kpah Sean Sherman na
kumuomba namba yake ya simu hii ni baada ya kukoshwa na mpira uliopigwa
na M-Liberia huyo.
No comments:
Post a Comment