PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Jul 18, 2015

YOUNG AFRICANS HISTORY IN KAGAME CUP || OPENING MATCH SINCE 1993


Ndugu wananchi, ni wazi na ukweli usiofichika kwamba hakuna mashabiki wanaofurahi timu yao kufungwa. Lakini kufungwa mechi ya kwanza ni NEEMA kuliko kufungwa mechi ya mwisho. Historia inainesha hivyo. Mechi za awali zinatuamsha usingizini kisha tunaanza kwenda kwa kasi kama treni inavyoshuka kutoka mlimani ikiwa imekatika breki.
- Nani kasahau kwamba msimu ulioisha tuliobeba Ubingwa tulianza kwa sare kisha tukacharazwa 3-0 na Mtibwa Sugar.
- Nani kasahau kwamba hata msimu kabla ya Azam FC kubeba ubingwa tulianza hivi hivi kwa kucharazwa na hao hao Wana-Manungu?

SASA TUANGALIE HISTORIA YETU YA KAGAME CUP
Mwaka 1993: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni Uganda, mechi ya kwanza tulifungwa 3-1 na wenyeji SC Villa tukakutana nao fainali tukawapiga 2 - 1, ndoo ikatua Jangwani.
Mwaka 1999: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni wale wale Uganda, mechi ya kwanza tulifungwa na Rayon Sports ya Rwanda mabao 3 - 0, tukaingia fainali na SC Villa tukashinda kwa penalties na shujaa akiwa ni Peter Manyika Sr. (Baba ake huyu kipa wa Mkia)
Mwaka 2011: Tanzania tukiwa wenyeji wa Kagame Cup, mechi ya kwanza tukatoa 2 - 2 na vigogo El Merreikh ya Sudan, tena magoli manne walifunga wachezaji wa El Merreikh. Fainali tukaingia na Wazee wa Mikataba Feki, tukawabanika 1 - 0, bao la Asamoah kufuatia krosi ya Kigi Makassy.
Mwaka 2012: Tanzania wakiwa wenyeji kwa mwaka wa pili mfululizo, mechi ya kwanza tukapigwa 2 - 0 na Atletico ya Burundi, Kavumbagu akiwa na timu hiyo akitupia na kutuadhibu. Fainali tukaingia Koni Chapati aka Azam FC tukawakalisha bao 2 - 0. Magoli ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi
Mwaka huu 2015: Tanzania wenyeji tena, mechi ya kwanza leo tumefungwa 2 - 1 na Gor Mahia ya Kenya.
WALE WANANCHI WOTE AMBAO BADO WANA IMANI NA TIMU YETU KAMA MIMI ADMIN WENU TUGONGE LIKE. WALE WASIO NA IMANI KAENI KIMYA TU.

No comments:

Post a Comment