PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Aug 27, 2015

RATIBA ZA MAKUNDI UEFA 2015-16

GROUP A
Paris(FRA)
Real Madrid(ESP)
Shakhtar Donetsk(UKR)
Malmö(SWE)


GROUP B
PSV(NED)
Man. United(ENG)
CSKA Moskva(RUS)
Wolfsburg(GER)

GROUP C
Benfica(POR)
Atlético(ESP)
Galatasaray(TUR)
Astana(KAZ)


GROUP D
Juventus(ITA)
Man. City(ENG)
Sevilla(ESP)
Mönchengladbach(GER)

GROUP E
Barcelona(ESP)
Leverkusen(GER)
Roma(ITA)
BATE(BLR)

GROUP F
Bayern(GER)
Arsenal(ENG)
Olympiacos(GRE)
Dinamo Zagreb(CRO)


GROUP G
Chelsea(ENG)
Porto(POR)
Dynamo Kyiv(UKR)
M. Tel-Aviv(ISR)

GROUP H
Zenit(RUS)
Valencia(ESP)
Lyon(FRA)
Gent(BEL)
Mechi za kwanza zitaanza tarehe 15-16 Septemba mwaka huu.

Aug 26, 2015

Mario Balotelli sitaki maneno nataka kufanya kazi


Mchezaji Mario Balotelli amejiunga na AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu akitokea timu ya Premier League ya Liverpool na haraka amesema hataki kuongea sana maneno zaidi ya kufanya kazi yake kwa bidii.
Balotelli amekuwa na msimu usiokuwa na mafanikio akiwa katika kikosi cha Brendan Rodgers, huku akishindwa kupasia nyavu za wapinzani na kuishia akiwekwa benchi kwa michezo mingi ya Premier League.
Je! Balotelli ataweza kurudisha makali yake yaliyoyeyuka akiwa na Liverpool!

Pedro:Nilikataa ombi la timu za Manchester


Mchezaji mpya wa Chelsea Pedro amefichua kwamba alikataa kujiunga na timu zote mbili za Manchester na badala yake kujiunga na Chelsea.
Winga huyo alifurahishwa na wazo la yeye kuhamia London baada ya kuamua kwamba angesalia Barcelona ili kuonekana katika picha.
Amesema kuwa alikataa ombi la kujiunga na timu hizo za Manchester huku akisema kuwa ushirikiano wa Jose Mourinho,Cess Fabregas na makao ya Stamford bridge ni baadhi ya vivutio vilivyomvutia.
Kilabu ya Manchester United ilikuwa kifua mbele katika kutafuta saini ya Pedro lakini ni Chelsea ilioharakisha uhamisho huo huku Mourinho na Fabregas wakihusika pakubwa katika kumrai ,mchezaji huyo.

Aug 20, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMIS 20.08.2015
Bayern Munich wamewaambia Manchester United kuwa kiungo Thomas Muller, 25 hauzwi, kufuatia taarifa kuwa wametoa dau la pauni milioni 60 (Manchester Evening News), Manchester United pia wamepata pigo jingine baada ya Southampton kusema hawamuuzi mshambuliaji wao Sadio Mane, 23 (Daily Star), Real Madrid wamekubali dau la pauni milioni 43 kutoka kwa Arsenal ili kumsajili Karim Benzima (Talksport), Wolfsburg watamuuza kiungo wao Kevin De Bryne, 24, kwenda Manchester City iwapo klabu hiyo itatoa pauni milioni 57 (Daily Mirror), West Ham wamejitoa katika kumfuatilia Emmanuel Abebayor kutoka Tottenham (Telegraph), West Brom wanajaribu kumsajili Federico Fazio, 28, kutoka Tottenham (Daily Mirror), mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 25, anatarajiwa kurejea Anfield mwishoni mwa wiki baada ya kukamilisha matibabu yake nchini Marekani, na huenda akacheza mechi yake ya kwanza, Septemba 12 dhidi ya Manchester United (Guardian). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

MAN UNITED WANAMNYATIA MANE( SOUTHHAMPTON)

Klabu ya Southampton ya Uingereza imakubali kuwa Manchester United wanavutiwa na wana mpango wa kumsajili winga kutoka nchini Senegal Sadio Mane. Ieleweke kwamba, United ilifanya jitihada kumapata mchezaji huyo mwenye miaka 23 tokea juma lililopita lakini Southampton wamekanusha kupokea ofa yoyote.
Mshambuliaji wa Barcelona Pedro amekuwa akihisiwa kujiunga na United lakini kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za kijiunga na Chelsea kwa dau la pauni milioni 21.
Mane alifunga magoli 10 katika michezo 32 aliyocheza msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu yake ya sasa akitokea Red Bull Salzburg ya Austria na yumo pia katika orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli matatu (hat-trick) kwa muda mfupi zaidi.

Aug 18, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 18.08.2015


Matamshi yaliyotolewa na kiungo Kevin De Bryne, 24 kuwa atabakia Wolfsburg msimu ujao yamepuuzwa na wakala wake na hivyo kuwepo bado na uwezekano wa uhamisho wa pauni milioni 50 kwenda Manchester City (Times), Chelsea wametoa dau jingine jipya la pauni milioni 30 kumtaka beki John Stones, 21, lakini huenda fedha hizo zikaongezeka kwa pauni milioni 10 zaidi ili kufanikisha uhamisho huo kutoka Everton (Telegraph), meneja wa Chelsea pia atapewa fedha zaidi na Roman Abramovich kununua wachezaji wengine wawili kabla dirisha la uhamisho halijafungwa kufuatia kuanza vibaya msimu mpya (Daily Mirror), Everton watamwania, ama- Ashely Williams, 30, wa Swansea au Kalidou Koulibaly, 24 wa Napoli, iwapo Stones ataondoka Goodison Park (Daily Star), Arsenal na Manchester United wametaarifiwa uwepo wa Zlatan Ibrahimovic, 33, ambaye ameambiwa na klabu yake ya PSG kuwa anaweza kuondoka kwa bei nafuu (Daily Mail), Manchester City wameambiwa waongeze dau kama wanamtaka beki wa Valencia Nicolas Otamendi (Sky Sports), City hawatomruhusu Eliaquim Mangala, 24, kwenda Valencia kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Otamendi (Daily Express), mkurugenzi mkuu wa Manchester United Ed Woodward amekwenda Barcelona kujaribu kukamilisha uhamisho wa Perdo (Daily Mail), Newcastle wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin kutokana na bei yake ya pauni milioni 15 (Newcastle Chronicle), hata hivyo West Ham bado wanataka kumsajili Austin (Evening Standard), Newcastle wanakaribia kumsajili winga wa Marseille Florian Thauvin, 22, katika mkataba ambao Remy Cabella, 25, atakwenda Ufaransa (Guardian), Juventus huenda wakamsajili Eric Lamela, 23, kutoka Tottenham iwapo watashindwa kumsajili Christian Eriksen, 23 (Evening Standard), Sunderland wanataka kumrejesha tena mchezaji kiraka wa Aston Villa Kieran Richardson, 30 (Daily Mirror), Southampton wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 24 kwa pauni milioni 8.5 na bado pia wanamtaka beki wa kati wa Celtic Virgil van Dijk (Daily Star), Sunderland wana wasiwasi watashindwa kumsajili Fabio Borini wa Liverpool na watazidiwa kete na Inter Milan (Sunderland Echo), West Brom wamepanda dau la pauni milioni 5 kumtaka Federico Fazio wa Tottenham (Telegraph), Norwich wanataka kumsajili Mattia Destro kwa mkopo kutoka Roma (Times), kipa wa Manchester United atatafakari kumfukuza kazi wakala wake Jorge Mendes iwapo hatofanikisha uhamisho wake kwenda Real Madrid kabla ya dirisha la usajili kufungwa

Aug 17, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 17.08.2015


Real Madrid watampa David De Gea, 24, pauni milioni 24 kama ada ya usajili, iwapo atamalizia mkataba wake ulosalia wa mwaka mmoja Old Trafford, wakati atakapoondoka bure msimu ujao (Daily Mirror), Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 28.5 wa beki wa Valencia Nicolas Otamendi, 27, huku Eliaquim Mangala, 24, akitarajiwa kwenda Spain kwa mkopo (Daily Mail), Manchester City wataongeza dau lao la pauni milioni 43 kumtaka kiungo wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne (Sky Sports), Tottenham wapo tayari wiki hii kutoa dau la pauni milioni 15 kumtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, huku beki Joleon Lescott, 33, kiungo Stephane Ssesegnon, 31, Brown Ideye, 26 na Victor Anichebe pia wakiruhusiwa kuondoka (Telegraph), dau la pauni milioni 5 kutoka Chelsea kumtaka beki wa Galatasaray Alex Telles limekataliwa (Daily Star), Everton watamnyatia beki wa Swansea Ashley Williams, 30, iwapo John Stones, 21, atakwenda Chelsea (Daily Star), meneja wa Everton Roberto Martinez pia anataka kumsajili mshambuliaji wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko (Liverpool Echo), meneja wa West Ham Slaven Bilic anamtaka kipa wa QPR Robert Green, 35, akitaka kuimarisha makipa wake (Sun), Newcastle na Everton wanamtaka beki Jannik Vestegaard, 23, wa Werder Bremen, lakini beki huyo anasema hana habari (Daily Express)

Aug 16, 2015

Jumatatu, 16 Agosti 2015



CHELSEA WAMEJARIBU KUPAKI BASI LAKINI IMESHINDIKANA

kocha wa chelsea alifikiri akimuweka kando daktari wa wachezaji (Eva Carneiro) ataweza kuibuka na ushindi. hii inonekana kwamba munrriho alikua amesha abiri matokeo. pamoja nakutumia mbinu mbalimbali lakini zote ziligonga mwambwa. mpaka mpira unakwisha Chelsea ilikuainaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 51. magoli ya city yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 31,Vincent Kompany dakika ya 79 na Fernandinho dakika ya 85

Aug 12, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 12.08.2015


Manchester United wameambiwa wasahau kumsajili Harry Kane, 22, huku Tottenham wakisisitiza kuwa hawatomuuza mshambuliaji huyo (Guardian), United huenda wakaweza kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pedro, 29, ambaye alipachika bao la ushindi katika mechi ya Supercopa, na amedaiwa kusema anataka kuondoka (Times), meneja wa Arsenal Arsene Wenger anafikiria kutoa pauni milioni 22 kumtaka kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak, 25 (Daily Telegraph), Manchester City wamemtaka Kevin De Bryne kutamka wazi kuwa anataka kuondoka (Manchester Evening News), Chelsea wanajiandaa kumsajili beki wa kushoto Abdul Rahman Baba, 21, kwa pauni milioni 17 (Sun), Sunderland watajaribu kumsajili winga wa Manchester United Adnaj Januzaj, 20, (Sunderland Echo), West Ham wameacha kumfuatilia kiungo wa zamani wa QPR Joey Burton, 32, baada ya mashabiki kumkataa (MIrror), Torino wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 kwa mkopo na baadaye moja kwa moja (Mirror), Schalke wamesema dau "kubwa sana" ndio litaweza kuwashawishi kumuuza kiungo wao Julian Drexler, 21 ambaye ananyatiwa na Arsenal na Manchester United (Daily Star), Aston Villa wanakaribia kumsajili winga kutoka Barcelona Adama Traore, 19, kwa pauni milioni 12 (Daily Mail), meneja wa Chelsea Jose Mourinho anasita kumuachia kiungo kutoka Brazil, Ramires, 28 kuondoka huku akinyatiwa na Juventus (London Evening Standard), QPR watampta mkataba mpya mshambuliaji wao Charlie Austin iwapo hakuna atakayeweza kumnunua kwa pauni milioni 15 (London Evening Standard)

KIKOSI CHA AZAM KITAKACHO KUTANA NA KMKM LEO

Kikosi kinachoanza leo dhidi ya KMKM ni
1.Mwadin Ali
2.Shomari Kapombe
3.Gadiel Michael
4.Abdallah Heri
5.Pascal Wawa
6.David Mwantika
7.Himid Mao
8.Mudathir Yahya
9.Ramadhan Singano
10.Shaaban Idd
11.John Bocco
Sub
1.Metacha Mnatha
2.Agrey Morris
3.Morad Said
4.Frank Domayo
5.Salum Aboubakar
6.Kipre Tchetche
7.Ammy Ali
8.Farid Musa
Not in today's game
1.khamis Mcha
2.Jean Mugiraneza
3.Erasto Nyoni
4.Didier Kavumbagu
5.Aishi Manula

LUIS SUAREZ KWENYE TUZO ZA UEFA

Mshambuliaji kutoka Uruguay, anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa Ulaya. Suarez anaungana na mshambuliaji mwenzake wa Barcelona Lionel Messi na vilevile katika orodha hiyo yuko hasimu wake Messi, Cristiano Ronaldo. Messi na Ronaldo walifunga mabao 77. UEFA wamesema wachezaji hawa watatu walipata kura nyingi zilizopigwa na waandishi wa habari kutoka katika orodha ya wachezaji kumi. Waandishi hao wa habari wapatao 54 ndio watamchagua mshindi wa tuzo hii ya mwaka 2014-15, tarehe 27 Agosti mjini Monaco. Siku hiyo pia ni ya droo ya Klabu Bingwa Ulaya.

Aug 11, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 11.08.2015

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 11.08.2015
Manchester City wametoa dau la pili la pauni milioni 47 kumtaka winga wa Wolfsburg, Kevin De Bryne, 24 katika jitihada zao za kusajili mchezaji wa tano msimu huu (Guardian), Everton watakataa dau la pauni milioni 30 kutoka Chelsea la kumtaka beki John Stones, 20 (Daily Mail), hata hivyo Everton wanafikiria kumfuata beki wa AC Milan Cristian Zapata, 28, kuziba nafasi ya Stones iwapo ataondoka (ESPN), Real Madrid wamewasilisha dau la mwisho la pauni milioni 21 kumtaka kipa wa Manchester United David De Gea, 24 (ABC), Stoke watamsajili kiungo wa Inter Milan Xherdan Shaqiri, 23 kwa pauni milioni 12 (Sun), Tottenham wamezidisha nia yao ya kumtaka mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 pamoja na Saido Berahino, 21, na wana uhakika wa kumpata japo mshambuliaji mmoja katika dirisha hili (London Evening Standard), Spurs pia wana matumaini ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Cameroon, Clinton N'Jie kutoka Lyon (Daily Telegraph), Tottenham pia wana nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Breel Embolo kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror), Liverpool wapo tayari kupokea dau kwa kiungo wao mkongwe Lucas Leiva, 28 (Liverpool Echo), Manchester United wamefikia makubaliano na beki kutoka Argentina Lucas Biliga, 29, na watamsajili kwa pauni milioni 17.7 kutoka Lazio (Le10Sport), matumaini ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos yamefifia tena baada ya beki huyo kushawishiwa na mkataba mpya wenye marupurupu yanayofikia pauni milioni 7.1 kwa mwaka (London Evening Standard), West Brom wanajiandaa kumsajili beki kutoka Spain Jose Enrique, 29 (Tuttomercatoweb), Everton huenda wanakaribia kumsajili beki wa Manchester United Jonny Evans, 27 (Metro), Chelsea wanakaribia kumsajili beki wa kushoto Baba Rahman, 21 katika mkataba utakaofikia pauni milioni 21.7 (Daily Express)
Barcelona vs Sevilla                 1-win

Luton Town vs Bristol City       2-win

Aug 10, 2015

HIKI NDIYO KIKOSI CHA BARCEONA KITAKACHO KUTANA NA SEVILA



 BARCA                                                            SEVILA

Marc-Andre ter Stegen
                                                                                     Sergio Rico Gonzalez
Gerard Pique
                                                                                      Benoit Tremoulinas
Daniel Alves
                                                                                      Grzegorz Krychowiak
Thomas Vermaelen
                                                                                      Thimothee Kolodziejczak
Jeremy Mathieu
                                                                                       Coke
Ivan Rakitic
                                                                                        Jose Antonio Reyes
Sergio Busquets
                                                                                        Vicente Iborra
Javier Mascherano
                                                                                        Ever Banega
Pedro Rodriguez
                                                                                        Vitolo
Luis Suarez
                                                                                        Michael Krohn-Dehli
Lionel Messi
                                                                                         Kevin Gameiro

Aug 8, 2015

YANGA KULIPIZA KISASI KWA AZAM

Mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki “Kagame Cup”, Azam FC inatarajia kuanza mazoezi leo Ijumaa asubuhi ikielekea Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi zaidi.

Azam FC inaingia msituni kujiwinda na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa mwishoni mwezi huu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall aliwapa mapumziko wachezaji wake mara tu baada ya kuchukua ubingwa huo uliowafanya waandike historia mpya kwani ni mara ya kwanza kutwaa Kombe hilo pia walicheza bila kuruhusu bao hata moja langoni mwao.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Dennis Kitambi alisema: "Tunatarajia kuanza mazoezi Ijumaa na baada ya hapo, tutaelekea Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi zaidi ya mechi yetu ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga."

"Sijajua ni siku kamili ya safari lakini inaweza kuwa Ijumaa hiyo hiyo jioni baada ya mazoezi au siku ya Jumamosi,"alisema Kitambi wakati wa halfla ya kumkabidhi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete kikombe.

Azam itacheza na Yanga mechi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi na Yanga ikiwa ni mabingwa.

RATIBA YA MECHI ZA JUMAMOSI, JUMAPILI NA JUMATANO


Aug 6, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMIS 06.08.2015


Tottenham wako tayari kumnyatia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin, 26, ambaye atagharimu karibu pauni milioni 15 (Daily Mirror), Spurs pia wanatarajia kuwazidi kete PSV na Atletico Madrid katika kumsajili winga kutoka Colombia Jeison Lucumi, 20, anayechezea America de Cali ya daraja la pili (Daily Mail), mshambuliaji mpya wa Manchester United Memphis Depay, 21, amemuambia meneja Louis van Gaal kuwa anataka kuvaa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa Angel Di Maria (Telegraph), nahodha wa Chelsea John Terry anaamini Chelsea itakuwa timu ya kwanza kutetea taji lake mfululizo katika kipindi cha miaka saba (Evening Standard), Real Madrid wanaweza kushawishiwa kumuuza Karim Benzima, 27, lakini Arsenal watalazimika kuvunja rekodi yao ya uhamisho kwa kutoa pauni milioni 45 (Daily Mail), Asier Illarramendi, 25, ameambiwa na Real Madrid kuwa hana nafsi ya kucheza katika klabu hiyo msimu huu na hivyo huenda akafikiria kuhamia Liverpool (Daily Express), Liverpool wanazungumza na Fiorentina kuhusu uhamisho wa Fabio Borini, 24 (Talksport), Angel Di Maria anatarajia kutangazwa rasmi kwa mashabiki wa Paris Saint-Germain leo (Daily Star), beki wa kushoto wa Augsburg Baba Rahman, 21, amekubali kuhamia Chelsea, lakini bado timu hizo mbili hazijakubaliana bei (Sky Sports), Manchester United wamepanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane (Daily Express), Nigeria imefanya juhudi za kumshawishi nyota chipukizi wa Liverpool Jordon Ibe, 19, kuichezea timu ya taifa ya Nigeria, badala ya England ambayo ameichezea katika ngazi ya vijana (Daily Mirror), Sergio Aguero, David Silva na Samir Nasri, huenda wakakosa mechi za mwanzo wa msimu baada ya kurejeshwa nyumbani kutoka mazoezini wakisumbuliwa na tatizo la tumbo (Daily Star), mshambuliaji wa zamani wa Liverpool El Hadji Diof, 34, ambaye anaichezea klabu iitwayo Saba ya Malaysia amesema anataka kuingia katika siasa atakapostaafu soka (Sun), uhamisho wa mkopo wa kiungo Leroy Fer wa QPR kwenda Sunderald umeshindikana baada ya mchezaji huyo kutopita vipimo vya afya (Independent), Saido Berahino huenda akasalia kuwa mchezaji wa West Brom, baada ya klabu hiyo kusema haijasikia lolote kutoka kwa Tottenham waliokuwa wakimnyatia (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez amepewa dau la dola milioni 10 na klabu moja ya ligi ya Marekani MLS, na amepewa saa 24 kuamua hatma yake (NBC Sports)

Aug 1, 2015

Azam FC imetinga hatua ya fainali za CECAFA Kagame Cup kwa mara ya pili baada ya kuichapa KCCA ya Uganda bao 1 - 0 na sasa itacheza fainali jumapili usiku katika dimba la uwanja wa taifa na Gor Mahia ya Keny.
Sifa zimwendee winga Farid Mussa aliyepachika bao hilo dakika ya 76 baada ya kupokea krosi nzuri ya Ame Ally. Katika mchezo huo ambao kwa mara nyingine beki , Muivory Coast Serge Wawa kachaguliwa kuwa mchezaji bora 'Man of the Match.
Azam FC ilikuwa ishangilie ushindi huo mapema kupitia kwa straika Muivory Coast Kipre Tchetche katika dakika ya 33 na 39 lakini ya mashuti yake kutoka nje.
Hata hivyo, mlinda lango, Aishi Manula alifanya kazi ya ziada dakika ya 36 alipookoa shuti la Sserunkuma Isaac ikawa kona tasa.
Azam FC ililiandama lango la KCCA baada ya kocha Stewart Hall kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Mudathir Yahya na naasi yake kuchukuliwa na Ame Ally, Erasto Nyoni akaingia Shomari Kapombe na Kipre Tchetche akaingia Didier Kavumbagu.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni/ Shomari Kapombe, Said Morrad, Aggrey Morris, Wawa, Mugiraneza, Mudathir Yahya/ Ame Ally, Domayo, Tchetche/ Kavumbagu, arid Mussa, John Bocco,

Matokeo | HJK Helsinki 0 - 2 Liverpool


Wachezaji Divock Origi na Philippe Coutinho wamefunga magoli katika maandalizi ya msimu mpya Premier League dhidi ya HJK.
Danny Ings alitoka na kuingia Divock Origi dakika ya 63 na kupata goli lake dakika ya 73.
Philippe Coutinho aliongeza goli la pili na kuwapa ushindi wageni hao na kumaliza ziara.
Toa comment zako kuhusu usajili mpya