PATA GARI LA BURE

PATA GARI LA BURE
bonyeza neno APPLY kwenye picha juu ujishindie gari

Aug 20, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMIS 20.08.2015
Bayern Munich wamewaambia Manchester United kuwa kiungo Thomas Muller, 25 hauzwi, kufuatia taarifa kuwa wametoa dau la pauni milioni 60 (Manchester Evening News), Manchester United pia wamepata pigo jingine baada ya Southampton kusema hawamuuzi mshambuliaji wao Sadio Mane, 23 (Daily Star), Real Madrid wamekubali dau la pauni milioni 43 kutoka kwa Arsenal ili kumsajili Karim Benzima (Talksport), Wolfsburg watamuuza kiungo wao Kevin De Bryne, 24, kwenda Manchester City iwapo klabu hiyo itatoa pauni milioni 57 (Daily Mirror), West Ham wamejitoa katika kumfuatilia Emmanuel Abebayor kutoka Tottenham (Telegraph), West Brom wanajaribu kumsajili Federico Fazio, 28, kutoka Tottenham (Daily Mirror), mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 25, anatarajiwa kurejea Anfield mwishoni mwa wiki baada ya kukamilisha matibabu yake nchini Marekani, na huenda akacheza mechi yake ya kwanza, Septemba 12 dhidi ya Manchester United (Guardian). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

No comments:

Post a Comment