Mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki “Kagame Cup”, Azam FC
inatarajia kuanza mazoezi leo Ijumaa asubuhi ikielekea Kisiwani Zanzibar
kwa ajili ya maandalizi zaidi.
Azam FC inaingia msituni
kujiwinda na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa
mwishoni mwezi huu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.
Kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall aliwapa mapumziko wachezaji
wake mara tu baada ya kuchukua ubingwa huo uliowafanya waandike historia
mpya kwani ni mara ya kwanza kutwaa Kombe hilo pia walicheza bila
kuruhusu bao hata moja langoni mwao.
Kocha msaidizi wa
Azam FC, Dennis Kitambi alisema: "Tunatarajia kuanza mazoezi Ijumaa na
baada ya hapo, tutaelekea Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi
zaidi ya mechi yetu ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga."
"Sijajua ni siku kamili ya safari lakini inaweza kuwa Ijumaa hiyo hiyo
jioni baada ya mazoezi au siku ya Jumamosi,"alisema Kitambi wakati wa
halfla ya kumkabidhi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya
Kikwete kikombe.
Azam itacheza na Yanga mechi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi na Yanga ikiwa ni mabingwa.
No comments:
Post a Comment