TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 11.08.2015
Manchester City wametoa dau
la pili la pauni milioni 47 kumtaka winga wa Wolfsburg, Kevin De Bryne,
24 katika jitihada zao za kusajili mchezaji wa tano msimu huu
(Guardian), Everton watakataa dau la pauni milioni 30 kutoka Chelsea la
kumtaka beki John Stones, 20 (Daily Mail), hata hivyo Everton
wanafikiria kumfuata beki wa AC Milan Cristian Zapata, 28, kuziba nafasi
ya Stones iwapo ataondoka (ESPN), Real Madrid wamewasilisha dau la mwisho
la pauni milioni 21 kumtaka kipa wa Manchester United David De Gea, 24
(ABC), Stoke watamsajili kiungo wa Inter Milan Xherdan Shaqiri, 23 kwa
pauni milioni 12 (Sun), Tottenham wamezidisha nia yao ya kumtaka
mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 pamoja na Saido
Berahino, 21, na wana uhakika wa kumpata japo mshambuliaji mmoja katika
dirisha hili (London Evening Standard), Spurs pia wana matumaini ya
kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Cameroon, Clinton N'Jie
kutoka Lyon (Daily Telegraph), Tottenham pia wana nafasi kubwa ya
kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Breel Embolo kwa pauni milioni 10
(Daily Mirror), Liverpool wapo tayari kupokea dau kwa kiungo wao mkongwe
Lucas Leiva, 28 (Liverpool Echo), Manchester United wamefikia
makubaliano na beki kutoka Argentina Lucas Biliga, 29, na watamsajili
kwa pauni milioni 17.7 kutoka Lazio (Le10Sport), matumaini ya Manchester
United kumsajili Sergio Ramos yamefifia tena baada ya beki huyo
kushawishiwa na mkataba mpya wenye marupurupu yanayofikia pauni milioni
7.1 kwa mwaka (London Evening Standard), West Brom wanajiandaa kumsajili
beki kutoka Spain Jose Enrique, 29 (Tuttomercatoweb), Everton huenda
wanakaribia kumsajili beki wa Manchester United Jonny Evans, 27 (Metro),
Chelsea wanakaribia kumsajili beki wa kushoto Baba Rahman, 21 katika
mkataba utakaofikia pauni milioni 21.7 (Daily Express)
No comments:
Post a Comment