Mshambuliaji
kutoka Uruguay, anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, ametajwa katika
orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa
Ulaya. Suarez anaungana na mshambuliaji mwenzake wa Barcelona Lionel
Messi na vilevile katika orodha hiyo yuko hasimu wake Messi, Cristiano
Ronaldo. Messi na Ronaldo walifunga mabao 77. UEFA wamesema wachezaji
hawa watatu walipata kura nyingi zilizopigwa na waandishi wa habari
kutoka katika orodha ya wachezaji kumi. Waandishi hao wa habari wapatao
54 ndio watamchagua mshindi wa tuzo hii ya mwaka 2014-15, tarehe 27
Agosti mjini Monaco. Siku hiyo pia ni ya droo ya Klabu Bingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment