Azam FC imetinga hatua ya fainali za CECAFA Kagame Cup kwa mara ya
pili baada ya kuichapa KCCA ya Uganda bao 1 - 0 na sasa itacheza fainali
jumapili usiku katika dimba la uwanja wa taifa na Gor Mahia ya Keny.
Sifa zimwendee winga Farid Mussa aliyepachika bao hilo dakika ya 76
baada ya kupokea krosi nzuri ya Ame Ally. Katika mchezo huo ambao kwa
mara nyingine beki , Muivory Coast Serge Wawa kachaguliwa kuwa mchezaji
bora 'Man of the Match.
Azam FC ilikuwa ishangilie ushindi huo mapema kupitia kwa straika Muivory Coast Kipre Tchetche katika dakika ya 33 na 39 lakini ya mashuti yake kutoka nje.
Hata hivyo, mlinda lango, Aishi Manula alifanya kazi ya ziada dakika ya 36 alipookoa shuti la Sserunkuma Isaac ikawa kona tasa.
Azam FC ililiandama lango la KCCA baada ya kocha Stewart Hall kufanya
mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Mudathir Yahya na naasi yake
kuchukuliwa na Ame Ally, Erasto Nyoni akaingia Shomari Kapombe na Kipre
Tchetche akaingia Didier Kavumbagu.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa;
Aishi Manula, Erasto Nyoni/ Shomari Kapombe, Said Morrad, Aggrey Morris,
Wawa, Mugiraneza, Mudathir Yahya/ Ame Ally, Domayo, Tchetche/
Kavumbagu, arid Mussa, John Bocco,
No comments:
Post a Comment